Kiungo Ousmane Dembele na Kylian Mbappe wote walifunga mabao mawili huku Paris St-Germain ikisogea hatua moja karibu na ubingwa wa ‘Ligue 1’.
PSG hata hivyo wanapaswa kusubiri kuthibitisha taji lao la tatu mfululizo baada ya Monaco kuwalaza Lille 1-0 katika mchezo uliofuata kupitia bao la Youssouf Fofana.
Ushindi wa PSG ulikamilika kati kati ya kipindi cha kwanza huku Dembele akitangulia kufunga kunako dakika ya 19 kabla ya Mbappe kufunga kwa shuti kali dakika tatu baadaye.
Mbappe alimpatia Dembele kwa mara yake ya pili ya mchezo, akitoa ustadi wa hali ya juu kwa kumzabaisha Nathaniel Adjei na kupiga mpira kwenye eneo la hatari kabla ya kuongeza hesabu yake mara mbili dakika za majeruhi.
Magoli ya nahodha huyo wa Ufaransa yalimfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ufaransa kufikisha 25 katika misimu minne mfululizo katika moja ya ligi tano bora Ulaya.
Faraja ya Lorient ilikuja wakati Bamba Dieng alipofunga kwa kichwa krosi ya Benjamin Mendy kati kati mwa kipindi cha pili.
PSG wangeliweza kumaliza siku wakiwa na uhakika wa ubingwa, lakini, ushindi wa Monaco kwenye mechi iliyofuata ulichelewesha sherehe zao.
Badala yake wanaweza kushinda ‘Ligue 1’ kwa mara ya 12 kesho mbele ya mashabiki wao wa nyumbani dhidi ya Le Havre.(AFP).