Skip to content

Kuhusu Zanzibarleo

Hii ni tovuti rasmi ya habari zinazotokana na Gazeti la Zanzibarleo linalomilikiwa na Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar.

Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS) Zanzibar limeanzishwa kwa Sheria Na. 11 ya mwaka 2008 likiwa na jukumu kubwa la kusimamia na kuzalisha magazeti ya Serikali.

Kama vilivyo vyombo vingine vya Serikali, SMS ni mdomo wa serikali na linafanya kazi za msingi za vyombo vya habari kwa ujumla ikiwemo kuelimisha, kuburudisha na kutoa habari kwa umma. Kupitia chombo hiki, sera, sheria, mikakati na mipango ya serikali inafafanuliwa kwa uwazi zaidi.

Shirika la Magazeti ya Serikali (SMS) linaendelea na kazi yake ya msingi ya kuchapisha magazeti ya Serikali yakiwemo gazeti la kila siku la Zanzibar Leo, gazeti la kila wiki la Zanzibar Mail pamoja na Zaspoti.  Magazeti haya pamoja na kuelimisha umma mambo mbali mbali yanayohusiana na uchumi, utamaduni na siasa za Zanzibar yanajumuisha pia taarifa nyingi ambazo zinahusu utalii, sekta ambayo ni tegemezi kwa Zanzibar.

Dira

Kuyafanya magazeti ya SMS kuwa kuwa ni bora na ya kisasa, yanayojitegemea na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Dhima

Kuhakikisha kuwa inajenga hadhi kubwa ya kuwatumikia wananchi katika misingi ya ukweli na kubeba dhamana ndani ya mfumo wa demokrasi na uhuru wa habari.

Huduma zetu

  • Kuchapisha habari katika vyanzo vyetu mbalimbali
  • Kuchapisha matangazo katika magazeti na mitandao yetu ya kijamii. Bonyeza hapa kuona viwango vya uchapishaji.

Magazeti Yetu