Skip to content

Barcelona yafikiria kumfukuza Xavi

BARCELONA, Hispania 

BARCELONA wanafikiria kumfukuza kocha mkuu, Xavi. 

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 alitangaza Januari kwamba angejiuzulu mwishoni mwa msimu, lakini, akashawishiwa kusalia na rais wa klabu, Joan Laporta. 

Hata hivyo, maoni ya Xavi katika mkutano na waandishi wa habari hivi majuzi yanaonekana kuikasirisha bodi ya klabu hiyo, ambayo sasa inahisi kiungo huyo wa zamani wa Hispania anapaswa kuondoka. 

Meneja wa timu ‘B’ ya Barcelona, Rafael Marquez ndiye anayependwa zaidi kuchukua nafasi ya meneja. 

Kabla ya ushindi wa wiki iliyopita ugenini dhidi ya Almeria, Xavi alieleza kuwa itakuwa vigumu kushindana kifedha na wapinzani wao Real Madrid na timu nyengine kuu barani Ulaya. 

Real tayari wametwaa ubingwa wa La Liga msimu huu, wapo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na watamsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kutoka Paris St-Germain majira ya joto. 

Barcelona wapo nyuma ya Real Madrid kwa pointi 14 kwenye ligi huku wakiwa wamebakisha michezo miwili. 

Xavi alichukua usukani Novemba 2021 baada ya kuondoka katika klabu ya Al Sadd ya Qatar na kuiongoza Barca kutwaa taji la Hispania katika msimu wake wa kwanza kamili wa kuinoa klabu mnamo 2022- 23.(AFP).